KAGERA SUGAR YAICHAPA RUVU SHOOTING 1-0 MOROGORO


BAO pekee la mshambuliaji Mganda, Hamisi Kizza ‘Diego’ dakika ya 90 limetosha kuipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi 32 na kusogea nafasi ya sita, wakati Ruvu Shooting inabaki na pointi zake 17 ikiendelea kushika mkia baada ya wote kucheza mechi 24.


Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON