CHELSEA YATINGA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA
WENYEJI, Chelsea FC wamefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund jana Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Mabao ya Chelsea jana yamefungwa na Raheem Sterling dakika ya 43 na Kai Havertz kwa penalti dakika ya 53 na kwa matokeo hayo Blues wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Ujerumani.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
