Mambo makuu mawili (2) ya kuyaepuka katika safari yako ya kimafanikio

Katika maisha ili uweze kufanikiwa zaidi yapo mambo ya msingi unayopaswa kuyaepuka ili uweze kufanikiwa zaidi, na mambo haya kama utaendelea kuyabeba ndivyo utakavyozidi kuwa maskini kila wakati.

Yafutazo ndiyo mambo ya msingi ya kuyaepeuka katika kuyasaka mafanikio:

1. Kuwalaumu watu wengine.
Hii ndiyo ile dunia ya lawama, maisha yetu yamejawa maneno kila kona, wengi wetu ni mabigwa sana wa kuwanyooshea vidole watu wengine huku tukidiliki kusema yeye ndiye aliyesababisha mimi kuwa hivi, huenda ni kweli yeye ndiye aliyesababisha kuwa hivyo ulivyo ila naomba nikwambie kwa kuwa hatma ya maisha yako unayo wewe hivyo unatakiwa kujifinza kuanza kuishi upya kwa kuchukua jukumu la kutekeza mambo yako mbalimbali ya mafanikio yatakayokusadia kuweza kupiga hatua za mafanikio.

2. Kuendela kununua vitu vilivyo nje ya uwezo wako.
Mara nyingi maisha yetu yanazidi kuwa magumu kila wakati hii ni kwasababu tumeendekeza vitu vilivyo nje ya uwezo wetu. Tunapenda kununua vitu vya ghari sana huku tukidhani labda ndio ujanja kumbe ni kujipoteza wenyewe pasipo sisi wenyewe kujua.

Wakati mwingine tujifunze kuacha vitu vingine vitupite tu, si kila kitu tunapaswa kukimiliki, kwani sisi uwezo wetu bado ni  mdogo basi tuendelea kununua vitu vya viwango vyetu huku tukiweka juhudi za kupata kile kikubwa tunachokihitaji.

Kila wakati unashauliwa kuwa kama uwezo wako ni wa kununua wali na maharahe basi  usihangake na na hayo mapizza na mabaga wanayokula wengine, tuwaachie wenye uwezo wa kuyanunua huku nasi tukiweka juhudi ya kuyapata haya mabaga na mapizza.

Wakati mwingine kuishi maisha ya kuonekana kwa watu wengine kama tunazo wakati hatuna kitu ni kujipoteza tu, usijifanye unazo pesa nyingi wakati hauna kitu, Kila wakati jifunze kuisha maisha ya uhalisia wako huku ukiweka juhudi thabiti na uadilifu uliotukuka katika kutimiza matakwa yako.

Mapambano dhidi ya umaskini yapo mikononi mwako hivyo  kila wakati jifunze mbinu mpya zitakazokusaidia sana kuweza kumili uchumi utakaokusaidia kukupa furaha na mafanikio kila wakati.

Na. Benson Chonya



Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON