Simba SC wapewa mbinu na Kocha wa Yanga SC


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mwinyi Zahera amewapa mbinu Simba ya kupenya katika hatua ya makundi kuelekea robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha huyo amewaasa Simba kutocheza kwa lengo la kusaka alama moja pekee ili waje kupambana kupata matokeo nyumbani Tanzania akiamini inaweza ikawa jambo gumu kwao.

"Simba wanapaswa kucheza kwa kufunguka, nimesikia kuwa wameenda na malengo ya kusaka alama moja pekee, si vema wakafanya hivyo maana inaweza ikawagharimu hapo baadaye, watafute ushindi na si alama moja" alisema.

Kauli ya Kocha huyo imekuja kufuatia Simba ambayo inaiwakilisha nchi, itakuwa na kibarua cha mechi hiyo kubwa kesho Jumamosi huko Kinshasa, Congo.

Zahera ambaye yuko mjini Shinyanga kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui, amewataka Simba kucheza mchezo wa kufunguka ili kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya AS Vita.

Tayari kikosi cha Simba kimeshawasili jijini Kinshasa jana na kilifanya mazoezi siku hiyohiyo tayari kujiweka sawa kuelekea kipute hicho.




Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON