HARUNA NIYONZIMA KUAGWA YANGA SC ALHAMISI KATIKA MECHI YA LIGI KUU TANZANIA BARA DHIDI YA IHEFU DAR

KLABU ya Yanga itautumia mchezo wake wa Alhamisi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ihefu SC kumuaga kiungo wake wa kimataifa wa wa Rwanda, Haruna Niyonzima.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na Haruna ataagwa Yanga baada ya kuitumikia tangu msimu wa mwaka 2011/2012 akiiwezesha kutwaa mataji manne ya Ligi Kuu, kabla ya kuhamia kwa watani wa jadi, Simba SC ambako pia alishinda mataji mawili.




Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON