ARSENAL YAICHAPA LEICESTER CITY 1-0 KING POWER


BAO pekee la  Gabriel Martinelli dakika ya 46 limeipa Arsenal ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Leicester City katika mchezo wa Ligi Kuu ya England leo Uwanja wa King Power Jijini Leicester, Leicestershire.
Kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 57 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya mabingwa watetezi, Manchester City baada ya wote kucheza mechi 24, wakati Leicester inabaki na pointi zake 24 za mechi 24 nafasi ya 14.


Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON