KAGERA SUGAR YAICHAPA NAMUNGO FC 1-0 KAITABA
BAO pekee la chipukizi Erick Mwijage dakika ya 79 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar ya kocha Mecky Mexime inafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya sita ikiizidi tu wastani wa mabao Namungo FC baada ya wote kucheza mechi 23.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
