BETIKA YALETA PROMO KUPELEKA MASHABIKI KUSHUHUDIA AFCON IVORY COAST


KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya Betika kwa kushirikiana na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo, imezindua Promosheni maalum ya kupeleka washindi wake kwenye michuano ya Kombe la Afrika ‘AFCON’ 2023 itakayofanyika Januari 13 hadi Februari 11 mwakani nchini Ivory Coast.
Katika michuano hiyo, timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepangwa Kundi F.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Betika, Juvenalius Rugambwa, alisema watanzania wakaobashiriki kupitia Betika kwa kushirikiana na Tigo wataenda nchini Ivory Coast kushuhudia mechi za Taifa Stars.
Alisema sasa wamekuja na promosheni hiyo baada ya kupita nyingine kubwa ambayo jumla ya mashabiki 400 kutoka mikoa mbalimbali walishuhudia mechi za watani wa jadi za Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Rugambwa alisema promosheni hiyo iliyopewa jina la ‘Twende Zetu Ivory Coast,KI VIP’ imenza rasmi na droo kubwa itafanyika Januari 2, kwa washindi 6 watapatikana ambapo washindi watapata huduma zote, kuanzia hapa nchini na hadi wakiwa nchini humo.
Alisema licha ya kuwepo kwa safari hiyo ya Ivory Coast, kuna zawadi mbalimbali za washindi ambapo televisheni nchi 70 kutoka Kampuni ya Hisense kila wiki kwa washindi wawili, zikiwa zimeambatana na king’amuzi, vikiwa vimeunganishwa na vifurishi vya mwezi mzima kutoka Kampuni ya Dstv na mamilioni kushindaniwa.
Kwa upande wa Meneja Biashara wa Tigo Pesa, Fabian Feliciana, alisema wao ni miongoni mwa wadau wakubwa wa soka wameona ni vizuri kushirikiana na Betika kuhakikisha washiriki wanacheza na kupata safari ya kwenda kushuhudia timu ya Taifa ikipeperusha bendera nchini Ivory Coast.
‘Tigo Pesa na Betika tunakwambia ‘Twende Zetu Ivory Coast,KI VIP’ ili uweze kujishindia safari hiyo weka pesa tigo pesa alafu ingia kwenye menyu ya *150*01,alafu utaingia namba 4 na kuweka no.545454, cheza Betika uende Ivory Coast KiVIP zaidi,” alisema Felician.                                                                     Katika michuano hiyo 24 zitachuana kuwania kuombe hilo ambapo Tanzania hii ni mara ya tatu kushiriki fainali hizo, Tanzania ipo pamoja na Morocco, DR Congo na Zambia, makundi mengin  (A) lina wenyeji  Ivory Coast, Nigeria, Equatorial Guinea, naGuinea-Bissau, Kundi( B)  zipo Misri, Ghana, Cape Verde na  Msumbiji.
Wakati  Kundi (C) zipo  Senegal, Cameroon, Guinea na  The Gambia, Kundi (D) Algeria, Burkina Faso, Mauritania na Angola na Kundi E kuna Tunisia, Mali, Afrika Kusini na  Namibia.


Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON