SIMBA SC YASHUSHA MUIVORY COAST KINARA WA MABAO ZAMBIA
KLABU ya Simba imemsajili mshambuliaji Muivory Coast, Freddy Michael Kouablan (25) kutoka Green Eagles ya Zambia ambako alikuwa anaongoza kufunga mabao kwenye Ligi Kuu ya nchi hiyo.
Huyo anakuwa mchezaji mpya wa tano dirisha hili dogo baada ya washambuliaji, Mgambia, Pa Omar Jobe (25) kutoka Zhenis ya Kazakhstani na Saleh Karabaka Kikuya (23) kutoka JKU ya ZanzĂbar.
Wengine ni viungo Msenegal, Babacar Sarr (26) kutoka US Monastir ya Tunisia na winga, Ladaki Juma Chasambi (19) kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

