Shonza atumia kauli ya Rais Magufuli kumuonya Gigy Money


Naibu wa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ameitumia kauli iliyotolewa na Rais Magufuli kuwaonya wale wanaotumia mitandao ya kijamii kuharibu maadili.

Shonza kupitia ukurasa wake wa Instagram ametumia kauli hiyo kumuonya Gigy Money na Wenzake ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii vibaya.

Rais alisema hivi “Mitandao ya Kijamii inaleta sana mmong’onyoko wa maadili, TCRA washughulikieni wanaotumia mitandao hiyo kuharibu maadili.”


Baada ya kauli hiyo, Shonza ameipost posti hiyo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusema " Walengwa natumai ujumbe wenu mmeishaupata kina @gigy_money_og na wenzio,msidhani hatuwaoni , “ashupazaye shingo yake atavunjika na wala hatapata dawa.”

Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON