TUZO ZA MCHEZAJI NA KOCHA BORA WA LIGI KUU ZAPATA MDHAMINI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitangaza kampuni ya Biko Sports kuwa Mdhamini wa tuzo za Mchezaji Bora na Kocha Bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
Biko Sports katika kipindi chote cha msimu wa 2018/2019 kilichobakia watatoa fedha kwa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora ambapo kila mmoja atapata shilingi milioni 1.
Mbali na fedha, Biko Sports watatoa tuzo kwa kocha na mchezaji bora wa kila mwezi.
TFF ina utaratibu wa kuwazawadia wachezaji bora na makocha wa kila mwezi pamoja na wale wa msimu mzima. 


Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON