GEITA GOLD YAICHAPA POLISI TANZANIA 1-0 NYANKUMBU
BAO pekee la mshambuliaji Elias Maguri dakika ya 25 limeipa Geita Gold ushindi wa 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 30 katika mchezo wa 21, ingawa inabaki nafasi ya tano ikizidiwa pointi 10 na Singida Big Stars ambayo pia ina mechi moja mkononi.
Kwa upande wao Polisi Tanzania hali bado ni mbaya, kwani baada ya kupoteza mchezo wa leo wanaendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16 wakibaki na pointi zao 14 za mechi 21.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
