BUSWITA AING’ARISHA NAMUNGO FC DHIDI YA DODOMA JIJI
BAO pekee la kiungo Pius Buswita dakika ya 56 limeipa Namungo FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Kwa ushindi huo, Namungo FC inafikisha pointi 14 na kusogea nafasi ya nane, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 15 nafasi ya saba baada ya wote kucheza mechi 12.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
