BABA SAMATTA AVUNJA UKIMYA, AAMUA HATMA YA MWANAYE AKITOKA GENK AENDE WAPI


Baba mzazi wa mshambuliaji wa KRC Genk, Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta atasimamia mwanaye atue ndani ya Ligi ya England na kuachana na ofa za nchi nyingine ambazo amezipata.

Samatta ambaye ndiye kinara wa mabao katika Ligi ya Ubelgiji amekuwa akihusishwa kutua katika klabu mbalimbali za England sambamba na Uturuki. Ofa ya juzi ni kutoka Cardiff City ambayo Genk waliipiga chini.

Mzee Samatta amesema anachotaka kuona ni mwanaye anatua England pekee na kuzipiga chini timu zingine zote ambazo hazishiriki EPL.

Kauli hiyo imekuja kufuatia timu lukuki ikiwemo zile za Spain kuanza kumfukzia nyota huyo ambaye amekuwa tegemo kwenye kikosi cha KRC Genk.

“Ninachotaka kuona ni kwamba Samatta anatua ndani ya nchi ya England na siyo kwingine ambapo wamekuwa wakimtaka wao aende.” alisema.

from SALEH JEMBE http://bit.ly/2CujKVV
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON