Halmashauri ya Arusha kuja na Operesheni Maalum kwa wasiolipa kodi

             

Halmashauri ya Jiji la Arusha kesho inatarajia kuanza Operesheni halali kufuatilia wasiolipa mapato ya Halmashauri ikiwemo ushuru, na tozo mbalimbali pamoja na kodi ya vibanda vinavyomilikiwa na Halmashauri hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Jiji la Arusha,  Dokta Seleman Madeni amesema operesheni hiyo itaanza kesho ikiwa na lengo la kuongeza pato la jiji kwa ajili ya maendeleo ya wakazi wa Arusha.

Amesema mwaka 2016/2017 walikuwa wakikusanya shilingi bilioni 13 ambapo wanatarajia kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kukusanya bilioni 15.

Dokta Madeni ameongeza kuwa Operesheni ya kuwatambua na kuwahakiki wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu Machinga waliochukua vitambulisho itafanyika mara baada ya kumaliza kuvitoa vitambulisho vyote 5,700.

Afisa biashara wa jiji la Arusha, Godfrey Edward ameelezea changamoto anazokabiliana nazo wakati wa ukusanyaji mapato,  huku akitoa angalizo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu machinga kuhusu vitambulisho vilivyotolewa na Rais John Magufuli.

Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON