HIGUAIN, MORATA, OZIL: TETESI KUBWA ZA SOKA BARANI ULAYA LEO ALHAMIS
Chelsea wameamua kumsajili Gonzalo Higuain baada ya Juventus kukubali ofa yao. Mshambuliaji huyo raia wa Argentina alikuwa akichezea AC Milan kwa mkopo. (Telegraph)
Atletico Madrid wanakaribia kumsaini mshambuliaji wa Chelsea lvaro Morata, 26, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 45. (Sky Sports)
Arsenal wako tayari kutumia sehemu ya mshahara wa Mesut Ozil endapo watafanikiwa kumuuza ili kumsajili mchezaji mwingine. Ozil ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi katika klabu hiyo. (Mirror)
West Ham wanapania kumnunua mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kujaza pengo litakaloachwa na Marko Arnautovic. (Sky Sports)
Manchester City huenda wakapoteza nafasi ya kumsajili Frenkie De Jong kutoka Ajax baada ya Paris St-Germain kuonyesha azma ya kutaka kumununua kiungo huyo.
Japo De Jong wa miaka 21 angelipendelea ujiunga city chini ya Pep Guardiola, PSG ndio klabu pekee ambayo iko tayari kulipa Ajax euro milioni 66. (Mirror)
Chelsea wanataka kumuuza mshambuliaji wao Michy Batshuayi, 25, kwa Everton kwa kima cha euro milioni 40.
Everton wanaweza tu kumsajili mshambuliaji huyo wa Ubelgiji kwa mkataba wa kudumu kwasababu tayari wamemsajili mlinzi wa Ufaransa Kurt Zouma, 24, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Star)
Batshuayi anataka sana kukamilisha mkopo wake ili aweza kuhamia Monaco. (Telegraph)
Kipa wa Uhispania David de Gea, 28, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya na Manchester United. (Mirror)
Wachezaji wa Chelsea Alvaro Morata, 26, na Olivier Giroud, 32, Fernando Llorente, 33 ,wa Tottenham, Lucas Perez, 30, wa Girona na Cristhian Stuani, 32, wa West Ham wako katika orodha ya Barcelona ya wachezaji wa ziada wanaotarajiwa kusajiliwa na klabu hiyo. (Mail)
Manchester United huenda wakamsajili winga wa PSV Eindhoven Steven Bergwijn huku wakiwa na lengo la kuweka dau la euro milioni 25 kumnunua kiungo huyo raia wa Ujerumani mwezi huu. (Sun)
De Gea huenda akawa bora zaidi Man Utd - Solskjaer
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Ubelgiji Divock Origi, 23, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Tottenham baada ya Harry Kane, 25, kuumia. (Telegraph)
Tottenham wamepanga mkutano wa ngazi ya juu kujadili jinsi watakavyo kabiliana na ukosefu wa Kane uwanjani kwa miezi kadhaa.
Kuna uwezekano wakawasaini wachezaji wapya au kumpandisha cheo mshambuliaji Troy Parrott mwenye umri wa miaka 16. (Talksport)
Kutoka BBC
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2RW0nyD
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
