Mbosso awaomba radhi mashabiki wake, kisa?


Msanii wa muziki Bongo kutokea lebo ya WCB, Mbosso amewaomba radhi mashabiki wake kufuatia kuchelewa kutoa video ya wimbo wake mpya.

Wimbo huo unaokwenda kwa jina la Tamu ulitoka December 22 mwaka jana lakini video yake rasmi
imekuja kutoka siku ya leo.

"Kwanza naomba radhi kwa kuchelewa kwa Video ya wimbo wenu huu pendwa, Tamu ni changamoto na mitihani ya hapa na pale ambayo ilikuwa nje ya uwezo wangu ilikwamisha kutoka kwa Wakati," ameeleza Mbosso.

Video hiyo imeongozwa na Director Kenny kutoka Zoom Production, hadi sasa wimbo huo umefikisha watazamaji (views) zaidi ya 20,000 ndani ya saa moja  tangu ilipotoka.



Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON