SAKATA LA KAKOLANYA NA YANGA LAIBULIWA TENA UPYA
Lile sakata la kipa wa Yanga aliyepigwa chini na Kocha Mwinyi Zahera limeibuka tena baada ya Mwanachama Mwandamizi, Edgar Chibula kuamua kuvunja ukimya.
Kwa mujibu wa Radio One, Chibula ameutaka uongozi wa Yanga kumfikiria Kakolanya kwakuwa bado ana mkataba na Yanga.
Mwanachama huyo ameeleza kuwa ni kweli Kakolanya alikosea lakini inabidi ifikie muda afikiriwe kama binadamu.
Ameongeza kuwa kipa huyo bado ana mkataba na Yanga na vilevile yupo katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars hivyo ni vema akafikiriwa upya.
"Ni kweli Zahera hana hamu ya kumsahe Kakolanya, lakini nauomba uongozi ujaribu kumfikiria mchezaji huyu kwa maana ana mkataba na vilevile anaichezea Taifa Stars" alisema.
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2QVTaKz
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON