RASMI, SIMBA SC MABINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA KWA MARA YA NNE MFULULIZO BAADA YA KUICHAPA COASTAL UNION 2-0
RASMI, Simba SC ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa nne mfululizo baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na washambuliaji, Nahodha John Raphael Bocco dakika ya 14 na Mkongo, Chris Kope Mutshimba Mugalu dakika ya 23.
Simba SC imefikisha pointi 79 baada ya mechi 32, tisa zaidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC kuelekea mechi mbili za mwisho za msimu, maana yake hata wakipoteza michezo hiyo hawawezi kufikiwa.
Hilo ni taji la nne mfululizo na la 22 jumla, sasa wanahitaji kutwaa mataji matano zaidi ili kuwafikia Yanga idadi ya kubeba ubingwa wa nchi, ambao wanaongoza baada ya kuchukua mara 27.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
