IHEFU YATINGA ROBO FAINALI AZAMS PORTS CUP
TIMU ya Ihefu imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Pan Africans leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya.
Mabao ya Ihefu SC inayofundishwa na makocha John Simkoko na Zuberi Katwila yamefungwa na Andrew Simchimba dakika ya 23 kwa penalti na dakika ya 47 akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Yacouba Sogne.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
