MBEYA CITY YAWATUPA NJE KAGERA SUGAR ASFC
BAO la mkwaju wa penalti la Richardson Ng’odya dakika ya 60 limeipa Mbeya City ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba leo.
Kwa ushindi huo, Mbeya City inakwenda hatua ya Robo Fainali ya michuano hiyo ikiungana na mabingwa watetezi, Yanga, Simba, Geita Gold, Ihefu SC, Mtibwa Sugar na Singida Big Stars.
Orodha ya timu za Robo Fainali itakamilika baada ya mchezo wa mwisho wa Hatua ya 16 Bora baina ya wenyeji, Azam FC na Mapinduzi ya Mwanza usiku wa leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
