SIMBA SC YASHINDA 4-0 NA KUTINGA ROBO FAINALI ASFC
WENYEJI, Simba SC wamefanikiwa kwenda Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Africans Sports ya Tanga leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Jean Baleke dakika ya 36, beki Kennedy Juma dakika ya 47, mshambuliaji Mzanzibari Mohamed Mussa dakika ya 69 na beki Jimmyson Mwanuke dakika ya 90.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
