BENO KAKOLANYA AFUNGIWA NA FAINI JUU KWA MATUSI NA UGOMVI


KIPA wa Singida Fountain Gate, Benno David Kakolanya amefungiwa mechi tatu na kutozwa Faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kujaribu kumshambulia kiongozi wa Coastal Union, Juma Kindo na kumtolea maneno machafu wakati wa mchezo baina ya timu hizo Novemba 27 Uwanja wa LITI, Singida.
Katika mchezo huo ambao Singida Fountain Gate walishinda 2-1, pia kama timu wametozwa Faini ya Sh. Milioni 1 kwa kosa la kuingia uwanjani wakati Coastal Union wanafanya mazoezi siku moja kabla ya mchez huo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.




Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON