MASHUJAA YAAMBULIA SARE 1-1 KWA TABORA UNITED KIGOMA


WENYEJI, Mashujaa FC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na jirani zao, Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.
Mashujaa FC walianza kupata bao kupitia kwa Jeremanus Josephat dakika ya 11, kabla ya Eric Okutu kuisawazishia Tabora United dakika ya 47.
Kwa ushindi huo, Mashujaa wanafikisha pointi tisa katika mchezo wa 10, ingawa wanabaki nafasi ya 15, wakati Tabita United inafikisha pointi 15 na kusogea nafasi ya saba baada ya kucheza mechi 11.


Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON