KUIFUATA SIMBA NI MILIONI 2


Simba imeondoka jijini Dar es Salaam jana asubuhi kwenda Kinshasa watakakocheza na AS Vita Jumamosi saa 1 usiku katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Lakini kama shabiki au mdau yeyote atataka kuifuata Simba nchini DR Congokwa ndege itamgharimu Sh 2,064,000 bila malazi.

Hiyo ni gharama ya usafiri wa ndege kwenda na kurudi pamoja na Visa ambacho ni kibali cha kukuruhusu kuingia kwao. Gharama za malazi ni kuanzia Sh160,000 kwenye hoteli nzuri ingawa zipo za gharama kubwa zaidi kutegemeana na kile anachotaka mhusika.

Usafiri wa ndege kuwahi mechi unapatikana leo na kesho ambapo kurudi ni siku ya Jumapili.

Tathmini iliyofanywa na gazeti la Spoti Xtra imebaini kwamba vitu ni ghali jijini humo kwa vile matumizi ya dola ya Marekani hayana tofauti na Faranga ya Congo, ambapo kwao wameshazoea kutumia dola kama fedha ya kawaida kutokana na ukubwa wa jiji hilo la kibiashara.

from SALEH JEMBE http://bit.ly/2RDD5Oy
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON