STAND UNITED WATOA KAULI YA KUTISHA KWA YANGA


KOCHA wa Stand United, Amars Niyongabo amesema kikosi chake kimejiandaa kiasi cha kutosha kuvuruga kasi ya vinara wa Ligi Kuu Bara Yanga.

Yanga wana pointi 53 wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 18 bila kupoteza hata mchezo mmoja, kesho watakuwa kibaruani kumenyana na Stand United Uwanja wa Karume, Shinyanga.

Niyongabo amesema wanawatambua wapinzani wao vizuri kwakuwa walicheza nao mzunguko wa kwanza hivyo ni wakati wa kuandika historia mpya kwa kupata ushindi.

"Tutakuwa nyumbani na tunatambua tunacheza na kikosi cha aina gani, wachezaji wana morali na wapo tayari kutibua rekodi ya wapinzani wetu Yanga.


"Kama wao wana rekodi nzuri basi nasi tuna wachezaji makini ambao watawazuia wasipate matokeo hapa, cha msingi waamuzi wazingatie kanuni 17 za mpira ili tusianze kutafutiana sababu," alisema Niyoganbo.



from SALEH JEMBE http://bit.ly/2Cr9jCc
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON