London Derby: Arsenal vs Chelsea
Arsenal Vs Chelsea, mchezo huu utapigwa katika dimba la Fly Emirates, majira ya saa 20:30 usiku.
| Mara ya kwanza | Chelsea 2–1 Arsenal 1907–08 Football League (9 Nov 1907) |
|---|---|
| Mechi ya mwisho | Chelsea 3–2 Arsenal (EPL) (18 Aug 2018) |
Arsenal, wameshinda mchezo moja kati ya michezo 14 ya ligi kuu England dhidi ya Chelsea, sare 5 amepoteza 8 Arsenal, mara ya mwisho kumfunga Chelsea, katika dimba la Emirates, ilikuwa mwaka 2016, kwa mabao 3-0.

Liverpool, ndo timu peke katika ligi kuu England wamepata clean sheet nyingi (13) msimu huu Chelsea, wanao wana clean sheet (10) arsenal, akiwa na clean sheet (3) na Fulham, ndo timu yenye clean sheet chache zaidi (2).
| Takwimu | |
|---|---|
| Magoli | 196 |
| Anayeongoza | Arsenal ameshinda mara 75 |
| Mfungaji bora | Didier Drogba (13) |
| Historia | Arsenal: mara 75 Sare: mara58 Chelsea: mara 63 |
| Kipigo kikubwa | Chelsea 6–0 Arsenal (22 March 2014) |
Arsenal, hajapoteza mchezo hata moja kati ya michezo 12 katika ligi kuu dhidi ya timu za mji wa London, katika uwanja wa nyumbani ameshinda mara 19 na amepoteza mara 3 pia ameshinda michezo mitano mfululizo ya mwisho dhidi ya timu za London, mara ya mwisho kupoteza dhidi ya Chelsea, katika uwanja wa nyumbani mwaka 2016.

Arsenal, wamefunga mabao 20 kwenye michezo 7 ya mwisho kwenye ligi kuu dhidi ya timu za mji wa London msimu huu ndo timu iliyofunga mabao mengi zaidi.
Chelsea, wanaangalia uwezekano wa kushinda michezo minne mfululizo kwenye ligi kuu katika viwanja vya ugenini mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa mwaka December, 2016 alishinda michezo sita.
MATAJI
| KIMATAIFA | Arsenal | Chelsea |
|---|---|---|
| UEFA Champions League | 0 | 1 |
| UEFA Europa League | 0 | 1 |
| UEFA Cup Winners’ Cup | 1 | 2 |
| UEFA Super Cup | 0 | 1 |
| Inter-Cities Fairs Cup | 1 | 0 |
| MAKOMBE YA NDANI | Arsenal | Chelsea |
| First Division / Premier League | 13 | 6 |
| FA Cup | 13 | 8 |
| League Cup | 2 | 5 |
| Full Members’ Cup | — | 2 |
| FA Community Shield | 15 | 4 |
| JUMLA | 45 | 30 |
Goli kipa wa klabu ya Arsenal Bernad Leno, amepata clean sheet moja katika michezo 15 ya ligi kuu aliyoanza msimu huu huku magoli kipa watatu ambao ni Gavin Ward, Julian Speroni, na John Ruddy, wao wote wamecheza michezo 15 hawajapata clean sheet.
Olivier Giroud, anaweza kuwa mchezaji wa pili kufunga akiwa na timu mbili tofauti kwenye ligi kuu England aliwahi kufanya hivo peke ni Cesc Fabregas, akiwa Arsenal na Chelsea.

Pierre Emerick, amehusika katika upatikanaji wa mabao 20 kwenye michezo 18 ya ligi kuu katika uwanja wa nyumbani mabao 15 na assist 5.
Azizi_Mtambo_15

from ShaffihDauda http://bit.ly/2ROYLXB
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON