MBABE WA EMMANUEL OKWI NA MEDDIE KAGERE AKWEA PIPA, MENEJA AFUNGUKA
MSHAMBULIAJI wa timu ya Mbeya City, Eliud Ambokile ambaye amefanikiwa kuwakalisha chini washambuliaji nyota wa timu ya Simba Emmanuel Okwi na Meddie Kagere amepata shavu la kufanya majaribio nchini Misri.
Ambokile mwenye mabao 10 mpaka sasa kwenye ligi akiwa amewaacha kwa idadi ya mabao matatu nyota wa Simba Okwi na Kagere huku kinara akiwa ni Heritier Makambo wa Yanga amekwea pipa leo kwenda Misri.
Kwa mujibu wa Meneja wa Ambokile, Gabriel Anthony amesema kuwa ana matumaini na mteja wake kufanya vizuri kwani lengo kubwa ni kuona anapata mafanikio kitaifa na kimataifa.
"Amekwenda Misri kwa ajili ya majaribio na akifanikiwa atajiunga huko hivyo taratibu zikikamilika kila kitu kitawekwa wazi kwa mashabiki wake kikubwa ni dua," alisema.
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2CuJrpa
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
