MBELGIJI WA SIMBA AWAPA DAKIKA TATU WACHEZAJI WAKE, ASISITIZA USHINDI KIMATAIFA
IMOOO ni neno ambalo limekuwa likitumika wakati mashabiki wakiwa na furaha ya kushangilia bao linalofungwa na timu yao Uwanjani.
Kwa sasa habari ya mjini ni namna ambavyo kikosi cha Simba kinazidi kupasua anga kimataifa Kwa kuonyesha ushindani wa kweli wakiwa ni vinara wa kundi D kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kundi D linajumuisha timu kama Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo na JS Saoure ya Algeria, wanaongoza kundi hilo kutokana na Kufunga jumla ya mabao matatu waliyoshinda.
Mpaka sasa Simba wanajumla ya mabao 15 kimataifa ambayo wamefunga katika mechi tano walizocheza Ila nyuma ya mabao hayo yupo Mbelgij Patrick Aussems ambaye ni Kocha Mkuu wa Simba.
Ana mengi ya kuwaambia mashabiki wa Simba juu ya mipango na harakati zake ndani ya Simba huyu hapa anafunguka:-
"Nafurahi kuona wachezaji wangu wanapata matokeo chanya katika michezo ambayo tunacheza ni Jambo gumu kulifikia Ila inawezekana kutokana na malengo ambayo tumejiwekea Kwa sasa.
Hesabu zako Kwa sasa zipoje kimataifa?
"Mpaka hapa tulipofika sio mbaya inaonesha namna gani tulivyo, tumeanza vizuri na tunahitaji kuendelea kupata matokeo kwenye michezo yetu yote.
Uwezo wa Waarabu ni kipimo sahihi kwa timu?
"Sina timu ya kubeza natambua madhara yake hivyo kuhusu kuwa kipimo ama sio kipimo mimi sijui, nachofikiria ni matokeo hakuna namna nyingine zaidi katika hilo, nimecheza nao umeona namna wanavyopambana kutafuta matokeo hivyo ni timu yenye ushindani.
Mechi tano mabao 15 kimataifa inamaanisha nini?
"Ushirikiano wa timu, kila mmoja anafanya kazi yake Kwa ukamilifu hali ambayo inatufanya tushinde na matokeo yanaonekana.
Timu inatengeneza nafasi nyingi inafunga mabao machache hili unalizungumziaje?
"Kweli hilo tatizo lipo na inatokea mara nyingi, safu yangu ya ushambuliaji huwa inakosa umakini hasa wakiwa eneo la hatari ni sehemu ya makosa ambayo nayafanyia kazi na nitafanikiwa katika hilo.
Mbinu ipi utatumia kutatua tatizo hilo?
"Mbinu mpya na nyepesi kwa washambuliaji wangu nawajenga kisaikolojia na kuwafanya wajiamini zaidi wakiwa eneo la hatari ili wapate tunachohitaji.
"Kwa kuanza nimeamua kuwafundisha wachezaji wangu wote namna ya Kufunga na hichi ndicho kinachotokea Kwa sasa ni mpango wa muda mrefu utakaoleta matokeo.
Nani akifunga anakufurahisha Kwa ufungaji wake?
Mbelgiji anacheka kisha anajibu "Wote wananifurahisha kwa namna wanavyofunga, sababu kubwa nawafundisha mbinu nyingi za Kufunga.
"Nataka wachezaji wangu wafunge kila aina ya mabao, watumie kichwa mguu wa kulia hata kushoto wafunge, pia hata Kwa kutumia sikio wafunge maana ushindi wetu umejificha kwenye mabao basi tunatakiwa Kufunga hamna namna nyingine.
Unatumia muda gani kufikiria kufanya mabadiliko ya wachezaji?
"Kwenye kila mchezo nagawa muda Kwa wachezaji na kutazama namna wanavyofanya kile nilichowaelekeza, ninaanza kipindi cha Kwanza Kwa kutazama dakika tatu za mwanzo mpaka kumi na tano tayari ninakuwa nimegundua makosa yao, hapo ndipo kama kuna ulazima nafanya mabadiliko.
"Muda mwingine inakuwa hauna hesabu za kufanya mabadiliko Ila inakulazimu hasa mchezaji anapopata majeruhi Ila kwangu mimi nina uhuru wa kufanya mabadiliko ndani ya dakika kumi na tano za mwanzo.
Wachezaji wako wamekuwa wakivimba ukiwatoa hilo lipoje?
"Nina wachezaji 18 ambao wanapaswa wacheze na wote wana uwezo sasa mchezaji mmoja ananipaje kiburi? Wote nataka wacheze waonyeshe uwezo wao nachohitaji ni ushindi na sio jina la mchezaji.
"Mtu kama Okwi najua anaujua mpira Ila muda mwingine anashindwa kufanya vizuri, hivyo anapaswa ampe nafasi mwingine huwa namuona anachukia akitolewa hilo nalijua na sijali tukipata matokeo tunaendelea kupambana naye anakuwa miongoni mwa wanaofurahia mafanikio hilo ndio la msingi kuliko mengine.
Huwa unawaambia nini wachezaji unaowafanyia mabadiliko wakitokea benchi?
"Tunahitaji matokeo nenda kafunge ukishindwa toa pasi ya bao unaweza nenda kafanye kazi.
"Najua tayari alikuwa akiona makosa ya wenzake hivyo anajua naye akikosea atatolewa inakuwa ni lazima aonyeshe utofauti na mwisho wa siku tunafanikiwa.
Mchezo wako ujao wa kimataifa unauzungumziaje?
"Utakuwa mchezo mgumu hasa ukizingatia tutakuwa ugenini Ila haitupi tabu, tumejiaandaa kiasi cha kutosha imani yetu tutafanya vizuri ni suala la muda.
Wachezaji wako morali yao ipoje?
"Wanajua kazi yao licha ya kutokuwa na kapten wao John Bocco bado wanakazi ya kufanya kimataifa, tupo sawa muda wote kupambana.
Nafasi ya Simba kimataifa unaiweka wapi?
"Kazi moja tu tuliyonayo na hicho ndicho tunachokifanya kupata matokeo Kwa kuwa hapa tulipo matokeo chanya ndio nafasi yetu hakuna kingine, nawaambia wachezaji ni ushindi Tu ushindi," anamalizia Aussems.
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2RzWUX8
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
