RUGU LA TFF HALIJAWAACHA SALAMA DARAJA LA KWANZA NA LIGI DARAJA LA PILI


KAMATI ya masaa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoa hukumu za makosa mbalimbali kwa waamuzi, wachezaji pamoja na timu kutoana na makosa yaliotafsiriwa ni utovu wa nidhamu.

Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kamati hiyo ilikutana na kuweza kupitia masuala mbalimbali ambapo baadhi yake wameyatolea ufafanuzi na mengine wamepeleka katika kamati nyingine.


Ligi Daraja la Kwanza

Mchezo wa Pamba dhidi ya green Warrior uliochezwa Januari 13, 2019, timu ya Green Warriors imepigwa faini ya laki tano kwa kile mashabiki wa timu yao kufanya vitendo vinavyoashiria imani za ushirikina. Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Pia klabu hiyo imetonzwa faini ya laki tano kutokana na baadhi ya mashabiki wao wakiongozwa na benchi la ufundi kuwazonga waamuzi huku wakiwatolea lugha chafu baada ya mchezo kumalizika. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Mechi namba 59- Januari 13, 2019: Mgambo Shooting 0 vs Geita Gold 1. Klabu ya Mgambo Shooting imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kuwa ndani ya uzio unaotenganisha wachezaji na mashabiki kwa muda wote wa mchezo, licha ya kutakiwa kuondoka. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Kwanza Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Ligi Daraja la pili

Mchezaji wa Mgambo Shooting, Dunstan D. Lipinga (jezi namba 30) anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumpiga Mwamuzi baada ya mchezo kumalizika. Pia mchezaji Rashid A. Shilla wa Mgambo (jezi namba 19) anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kumpiga Meneja wa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Mechi namba 17- Novemba 18, 2018: Mtwivila 0 vs The Mighty Elephant 0. Klabu ya The Mighty Elephant imepewa Onyo Kali kwa kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mchezo (technical meeting) bila kutoa taarifa yoyote kwa Kamishna. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo.

Pia The Mighty Elephant imepigwa faini ya sh. 200,000 (laki mbili) kwa kuchelewa kufika uwanjani kwa dakika 20. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(48) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Utaratibu wa Mchezo.

Mechi namba 18- Novemba 18, 2018: Kitayosce 0 vs Kilimanjaro Heroes 0. Kocha wa Kitayosce, Hamad Haule amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kuondolewa kwenye benchi kwa kosa la kuongea na simu hata baada ya kukatazwa na Mwamuzi wa akiba. Adhabu imezingatia Kanuni ya 41(11) ya Ligi Daraja la Pili Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Pia Mtunza Vifaa wa Kilimanjaro Heroes, Noel Paul anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kuondolewa kwenye benchi kwa kosa la kuongea na simu, licha ya kukanywa asitumie simu lakini alikaidi.

Mechi namba 27- Januari 5, 2019: Kitayosce 1 vs Mtwivila 1. Kocha wa Mtwivila, Lisa Mwalupindi amefungiwa mechi mbili na kupigwa faini ya sh. 300,000 (laki tatu) baada ya kuondolewa kwenye benchi kwa kupinga mwamuzi ya Mwamuzi. Adhabu imezingatia Kanuni ya 41(11) ya Ligi Daraja la Pili Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Makocha.

Naye Daktari wa Kitayosce, Michael Evarest anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kutolewa kwenye benchi la ufundi kwa kosa la kuchelewesha kuanzishwa kwa mchezo baada ya kuamriwa na Mwamuzi atokee sehemu ya karibu alikaidi na kutokea sehemu ya mbali.

Mechi namba 18- Novemba 17, 2018: Bulyanhulu 0 vs Kasulu Red Star 0. Meneja wa Kasulu Red Star, Kapama Kapama anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kutoa lugha ya matusi kwa Mwamuzi.

Mechi namba 28- Januari 6, 2019: Milambo vs Madini SC. Timu ya Madini SC imeshushwa madaraja mawili kwa kutofika uwanjani. Hivyo, matokeo ya mechi zote ilizocheza yamefutwa ili kutoa uwiano sahihi kwa timu zilizobaki kwenye Ligi.

Pia timu hiyo imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili). Adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 28 (1) na (2) ya Ligi Daraja la Pili Toleo la 2018 kuhusu Kutofika Uwanjani.

Mechi namba 25- Januari 5, 2019: Cosmopolitan 1 vs Changanyikeni 0. Klabu ya Changanyikeni imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na washabiki wa timu yao kumpiga Mwamuzi huku wakimtolea lugha ya matusi. Adhabu imezingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Daraja la Pili Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Mmiliki wa timu ya Changanyikeni, Omar Bawazir anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kuingia uwanjani na baadhi ya washabiki na kumpiga Mwamuzi.

Vilevile Mwamuzi wa mechi hiyo, Ibrahim Mohamed ameondolewa kwenye Orodha ya Waamuzi wa SDL baada ya kupata alama za chini.

Mechi namba 27- Januari 6, 2019: African Sports 0 vs Forest 2. Malalamiko ya African Sports kuwa usajili wa wachezaji Timotheo Emmanuel Kombo na Lawrence Milton Mganga wa Forest si halali yamekataliwa. TFF imethibitisha kuwa wachezaji hao wamesajiliwa kihalali kwenye timu ya Forest.


from SALEH JEMBE http://bit.ly/2R339he
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON