Zahera asema ili Simba iwafunge Vita ni lazima wafanye haya

Zahera asema ili Simba iwafunge Vita ni lazima wafanye haya

Kocha Mkuu wa Timu ya Yanga Zahera Mwinyi ambaye ni raia wa Congo na anaijua vyema klabu ya AS Vita ametoa maoni yake kuelekea pambano kati ya Simba na AS Vita siku ya Jumamosi 19 January 2019 huko Kinshasa.

Zahera alisema ili Simba iweze kushinda ni lazima wacheze mchezo wa Kushambulia na siyo wa kujilinda kama kweli wanahitaji kupata matokeo.

Wachezaji 18 Yanga walioenda Shinyanga kuivaa Stand United

Zahera alisema Simba wanatakiwa waende wakiwa na akili ya kushambulia na kutafuta ushindi na siyo kuingia wakiwaza sare kwani wanawachezaji wazuri wanaoweza kuwapa matokeo.

Aliwashauri wacheze kama walivyocheza na timu ya Js Saoura kwa kushambulia muda wote wa mchezo ila wakienda tofauti na hapo basi wanaweza kuchezea kichapo

Pata Maujanja ya wakubwa Tu hapa

The post Zahera asema ili Simba iwafunge Vita ni lazima wafanye haya appeared first on KWATA UNIT Sports News.



from KWATA UNIT Sports News http://bit.ly/2CurXcF
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON