Matokeo Simba U-20 vs Cameroon U-17

Matokeo Simba U-20 vs Cameroon U-17

Leo kikosi cha Simba chini ya Miaka 20 kilikuwa na kazi ya kupimana ubavu na timu ya Cameroon U-17, Cameroon wakiwa wanajiandaa na michuano ya AFCON U-17 yatakayofanyika Tanzania kuanzia 14 April 2019.

Pambano hilo limemalizika kwa dakika 90 timu hizo kutoa sare ya bao 1 kwa 1 huku mechi ikiwavutia watu wengi kutokana na wachezaji wa timu zote mbili kuonyesha kiwango safi.

Cameroon U-17 ndiyo waliokuwa wa Kwanza kupata bao , bao lililodumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika huku Simba U-20 wakirudi kipindi cha pili kwa nguvu na kusawazisha dakika ya 52 kupitia kwa Salum Mkeyenge

The post Matokeo Simba U-20 vs Cameroon U-17 appeared first on KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT.



from KWATA UNIT SPORTS & ENTERTAINMENT http://bit.ly/2Ic7dLW
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON