Rais Magufuli atoa siku 30 kukamilishwa kwa Ujenzi wa Kituo cha Mabasi
Na Amiri kilagalila-Njombe
Rais John Pombe Magufuli ameiagiza Serikali mkoani Njombe kwa kushirikiana na Wizara ya ujenzi na uchukuzi kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Mabasi ndani ya siku 30 kufuatia ujenzi huo kuchukua zaidi ya miaka 7 na kusababisha kuwa kero kwa wananchi ambao bado wanatumia kituo cha zamani ambacho ni kidogo na hakina miundombinu bora.
Rais magufuli wakati akizungumza na wananchi mkoani njombe katika Uwanja wa sababa ameagiza pia bodi ya wakandarasi kumchunguza mkandarasi anayejenga kituo hicho cha mabasi katika awamu ya kwanza na ya pili kutoka kampuni ya masasi constructioni na kusababisha kuto kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho
“wameshazungumza hapa tarehe 20 watakabidhi mimi nimeongeza siku 10 zingine kwa hiyo iwe tarehe kumi mwezi wa tano wakabidhi na stendi iwe imemalizika kwa kiwango kinachotakiwa,lakini msajili wa bodi muanze kumchunguza huyu masasi construction mkatumie sheria namba 17 ya mwaka 1997 ambayo sheria ile inaruhusu hata kufungwa miaka mitano mkaisome vizuri kama hafiti kuwa contractor mkamfute kabisa akafanye kazi nyingine”alisema Magufuli
Awali akizungumza kucheleweshwa kwa stendi hiyo mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata mwenda alisema kuwa serikali imetoa fedha zote kwa ajili ya ujenzi wa stendi ile lakini imecheleweshwa na mkandarasi wa kwanza.
“Kwanza nichukue nafasi hii kushukuru kwamba umeweza kutupata fedha zote za ujenzi wa awamu ya kwanza na awamu ya pili na tumeweza kujenga stendi hii kwa awamu ya kwanza mwaka 2013 tumejenga mpaka 2015 tukaingia awamu ya pili na awamu ya pili mkandarasi akawa amechelewesha kazi na mwaka 2017 -2018 mwishoni tukaamua kumtoa mkandarasi Yule tukamuweka mwingine na sasa hivi stendi imekwishafikia asilimia 80 na kabla ya june stendi ile itakuwa tayari”alisema BI.Mwenda
Stendi ya Njombe mjini iliyoanza mwaka 2013 ambayo mpaka sasa haijakamilika na kufikia zaidi ya miaka 7 inagharimu zaidi ya shilingi bilioni 9 ili kuweza kukamilika.
Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
