YONDANI KUKOSA MECHI TATU LIGI KUU NA FAINI YA LAKO TANO


Beki kisiki wa Young Africans Kelvin Yondani sasa atakosa jumla ya mechi tatu zijazo katika ligi

Adhabu hiyo atakubana nayo kufuatia kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwenye mchezo wa jana dhidi ya Kagera sugar uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-2.

Beki huyo atakosa mechi hizo kwa kosa la kupiga kiwiko mchezaji wa Kagera na kupelekea kulimwa kadi hiyo.

Kwa mujibu wa kanuni za wanaoendesha mpira, Yondani atakosa michezo mitatu mfululizo ya Yanga SC ama kupigwa faini sh.500,000.

Michezo mitatu atakayoikosa beki huyo kisiki nchini ni dhidi wakata miwa wa Mtibwa Sugar ambao utachezwa Morogoro (17 April 2019) Azam FC vs Yanga (29 April 2019) na Mchezo wa FA dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Iringa.

from SALEH JEMBE http://bit.ly/2G77ix9
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON