Waziri Mkuu wa Bahrain afariki
Waziri Mkuu wa Bahrain Khalifa bin Salman al-Khalifa ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 84.
Kulingana na taarifa zilizotolewa na vyanzo rasmi vya habari nchini Bahrain, iliripotiwa kuwa al-Khalifa alifariki katika hospitali aliyokuwa akipokea matibabu nchini Marekani.
Mamlaka kuu ya Kifalme ya Bahrain imetangaza kuwa mazishi ya Waziri Mkuu yatafanyika na kuhusisha washiriki wa familia pekee.
Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
