BUCKS YAIBWAGA PHOENIX SUNS 123-119 MECHI YA TANO FAINALI NBA

TIMU ya Milwaukee Bucks imeibuka na ushindi wa 123-119 dhidi ya Phoenix Suns katika mechi ya tano ya Fainali za Ligi ya Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) Alfajiri ya leo ukumbi wa  Footprint Center, Phoenix, Arizona. 
Pongezi kwao, Giannis Antetokounmpo aliyefunga pointi 32, rebounds tisa na assists sita, Khris Middleton pointi 29 na Jrue Holiday pointi 27 na assists 13.
Sasa Milwaukee Bucks inaongoza kwa ushindi wa mechi 3-2 baada ya mwanzo mzuri wa Phoenix Suns kuongoza 2-0 baada ya mechi mbili za mwanzi na wakishinda mechi ya sita Alfajiri ya Jumatano nyumbani, watatwaa taji la kwanza la NBA 1971.



Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON