MIDDLETON ANG'ARA, BUCKS YASAWAZISHA, 2-2 NA SUNS FAINALI NBA

FORWARD Khris Middleton amefunga pointi 40, zikiwemo 10 straight, Giannis Antetokounmpo akaongeza pointi 26, rebounds 14 na assists nane kuiwezesha Milwaukee Bucks kufufua matumaini ya ubingwa wa NBA baada ya ushindi wa 109-103 dhidi ya Phoenix Suns na sasa kila timu imeshinda Sereis mbili (2-2).
Upande wa Suns, Devin Booker alifunga pointi 42, lakini faulo zake zikawagharimu kipindi  cha pili na mkongwe Chris Paul amefunga pointi 10 tu na turnovers tano.
Game 5 itafuatia Jumapili (Julai 18) huko Phoenix kuanzia Saa 10:00 Alfajiri, Game 6 Julai 21 na Game 7 Julai 23 #ESPN2. 




Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON