GEITA GOLD NA NAMUNGO ZASONGA MBELE KIBABE AZAM FEDERATION CUP
TIMU ya Geita Gold imefanikiwa kutinga Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Singida Cluster katika mchezo uliofanyika leo Uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu mjini Geita.
Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Tariq Seif dakika ya 14 na 19, Mwaita Gereza dakika ya 47, George Sangija dakika ya 49 na Geofrey Julius dakika ya 90 na ushei.
Mechi nyingine za ASFC leo, Namungo imeitupa nje Hollywood kwa kuichapa mabao 5-0 Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi.
Mabao ya Namungo FC yamefungwa na James Mwashinga dakika ya 23, Kelvin Sabato dakika ya nane kwa penalti, 36 na 63 na Michael Joseph dakika ya 77.
Nayo Tabora United imeichapa Coffee ya Mwadui 4-1 Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora huku jirani zao, Mashujaa FC wakiilaza Mbuga FC 3-2 Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Chanzo: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
