AZAM FC WAISHANGAA BODI YA LIGI, WAITAJA YANGA
UONGOZI wa Azam FC umeishangaa Bodi ya Ligi kuwaruhusu waanze kucheza mzunguko wa pili kabla ya kumaliza viporo vyao walivyonavyo mkononi.
Azam imecheza mechi 18 ikiwa imesaliwa na mechi mbili za mzunguko wa kwanza dhidi ya Yanga na Simba, kesho itakuwa na kibarua mbele ya Mwadui FC mchezo ambao utapigwa Uwanja wa Chamazi.
Ofisa habari wa Azam, Jaffar Maganga amesema wao walitakiwa kucheza na Yanga kwa sasa ambao wapo hapa tofauti na Simba ambao wanamajukumu mengine ya kimataifa.
"Tulitarajia ratiba ingewekwa wazi juu ya mechi zetu za Simba na Yanga tutacheza lini kabla ya kuanza mzunguko wa pili, mambo yamegeuka tumeanza kucheza mechi za mzunguko wa pili kitu ambacho si sahihi.
"Tulitakiwa kucheza na timu hizo kama Yanga kwa sasa ipo hapa tulikuwa na uwezo wa kucheza nayo ila bodi ya ligi wameshindwa kuweka ratiba bora, hata Simba ambao hawapo hapa kutokana na michuano ya kimataifa inabidi vyombo husika vijipange katika hili," alisema Maganga.
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2CuJ0ew
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
