KAMA UNADHANI SIMBA WAMEENDA KUSAKA ALAMA MOJA KWA WAZEE WA SEBENE, MSOME AUSSEMS HAPA
Kocha Mkuu wa klabu ya Simba, Patrick Aussems, amesema mechi yao ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita haitakuwa rahisi.
Simba itakuwa mgeni dhidi ya Vita Jumamosi hii ambapo mechi hiyo itakuwa ni ya aina yake kutokana an timu zote mbili kuwa na rekodi nzuri msimu huu kwenye mashindano hayo.
Aussems amefunguka kuwa Simba haijaenda Congo kwa ajili ya kuzuia na badala yake wameenda kusaka ushindi ili kufanikisha kutinga hatua ya robo fainali.
Tayari maandalizi kuelekea mechi hiyo yanaendelea ambapo Simba inaenda kukipiga na wazee hao wa sebene ikiwa na kumbukukumbu ya kuwanyoosha waarabu JS Saoura kwa mabao 3-0 Dar.
"Itakuwa mechi ngumu lakini hatujaja hapa kuzuia, tumekuja hapa kujaribu kutengeneza nafasi kama ilivyo kwa michezo yetu mingine na kujaribu kufunga."
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2RCU1Fb
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
