RUNGU LA KAMATI YA MASAA 72 LATUA KWA WAAMUZI WA SIMBA, KOCHA SINGIDA UNITED


KAMATI ya masaa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetoa hukumu za makosa mbalimbali kwa waamuzi, wachezaji pamoja na timu kutoana na makosa yaliotafsiriwa ni utovu wa nidhamu.

Ofisa Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura amesema kamati hiyo ilikutana na kuweza kupitia masuala mbalimbali ambapo baadhi yake wameyatolea ufafanuzi na mengine wamepeleka katika kamati nyingine.

 Wambura amesema adhabu hizo na mashauri mengine yamefanywa baada ya kamati ya uendeshaji wa ligi kuweza kupitia malalamiko na matukio tofauti ambayo yaliweza kutokea katika mechi tofauti zile za ligi kuu, ligi daraja la kwanza na la pili katika michezo yao hivi karibuni.


"JKT Tanzania walileta malalamiko yao juu ya mchezo wao na Simba malalamiko yamepitiwa na mwamuzi Mbaraka Rashid amepewa onyo kali kutokana na kutokuwa makini, msaidizi wake Mashaka Mwandebwa amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea.

"Wachezaji wa Singida United Geodfrey Mwashiuya amefungiwa mechi tatu baada ya kumpiga mchezaji wa Biashara United huku Rajab Zahiri katika mchezo huohuo alitaka kumpiga mwamuzi wa mchezo  hivyo kafungiwa mechi tatu, kocha wao Shadrack Nsajigwa amefungiwa mechi mbili na faini ya laki tano kwa kujibizana na mwamuzi.

"Mchezo kati ya Simba na Singida United, Singida wamepigwa faini ya laki mbili baada ya kushindwa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo na kwenda chumba cha media centre ambapo sio eneo sahihi pia katika mchezo kati ya Yanga na Ruvu Shooting mtunza vifaa wa Ruvu Augustine Kalangwa amepelekwa katika kamati ya nidhamu.

Mashabiki na wachezaji wanapaswa watambue kwamba ni wajibu wao kufuata taratibu zilizowekwa bila kukiuka endapo kutakuwa na ukiukwaji hatua kali dhidi yao zitachukuliwa bila kuwasahau waamuzi wanapaswa watende kazi kwa weledi," alisema Wambura



from SALEH JEMBE http://bit.ly/2RCLJNh
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON