JKT QUEENS WABABE KINOMA WAIVURUGA SIMBA QUEENS
Ligi Kuu ya Wanawake ambayo inashirikisha timu 12 mpaka sasa timu zote zimeshacheza michezo sita na zimefanikiwa kuweka rekodi yao ila JKT Queens mpaka sasa wamefanikiwa kuweka rekodi tamu.
Katika michezo sita wamefanikiwa kushinda michezo sita na kujikusanyia pointi 18 wakiwa ni vinara kwenye Ligi hiyo hawajaruhusu nyavu zao kutikishwa mpaka sasa na timu yoyote ile.
Yanga Princess ambao wamepanda daraja msimu huu wameanza vizuri kwani katika michezo sita waliyocheza mpaka sasa wamefanikiwa kushinda michezo miwili na kujikusanyia pointi sita abazo zinawaweka nafasi ya saba tofauti na Evergreen Queens na Mapinduzi Queens ambao katika michezo sita hawajafanikiwa kushinda hata mchezo mmoja.
Simba Queens walikuwa wakipewa nafasi ya kumtungua JKT Queens wamebadilishiwa gia baada ya kucheza michezo sita wamepoteza mmoja na sare mchezo mmoja unaowafanya wajikusanyie pointi 13 nafasi ya tatu kwenye Ligi wakishushwa nafasi ya pili na Mlandizi Queens ambao hawajapoteza mchezo wana pointi 16.
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2W6gxF5
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON