ZAHERA AMBEBESHA ZIGO ZITO MSHAMBULIAJI HUYU YANGA, AMHAKIKISHIA KUANZA KIKOSI CHA KWANZA


BAADA ya kurejea nchini Tanzania akitokea nchini Congo kutokana na matatizo yake ya kifamilia, mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo leo anaanza kazi yake mbele ya wapinzani wa Stand United.

Makambo ni kinara wa upachikaji mabao kwenye msimamo wa wafungaji Ligi Kuu Bara akiwa amefanya hivyo mara 11 leo amepewa jukumu la kuiangamiza Stand United.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema ameridhishwa na uwezo alioonyesha Makambo kwenye mazoezi yao ya mwisho hali inayomfanya aamini kwamba ana nafasi ya kuanza kucheza leo.

"Nimemuona Makambo akiwa kwenye mazoezi, tayari ameonesha ubora wake hali ambayo inanifanya nimuamini na nitampa majukumu mapya leo kwenye mchezo wetu dhidi ya Stand United," alisema Zahera.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza waliocheza Uwanja wa Taifa, mchezo ulimalizika kwa Yanga kushinda mabao 4-3 dhidi ya Stand United.


from SALEH JEMBE http://bit.ly/2R1RyPv
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON