BODI YA LIGI WAJA NA MAAMUZI MAPYA KUHUSIANA NA VIPORO VYA SIMBA
Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema watafanyia kazi viporo vya Simba ambavyo vimezidi kuwa vingi kutokana na ushiriki wao katika mashindano ya kimataifa.
Kauli ya Wambura imekuja kufuatia mjadala ambao unazidi kushika kasi dhidi ya viporo hivyo ambavyo kwa namna moja ama nyingine vinatajwa kupunguza ladha ya ligi.
Kiongozi huyo amesema wataandaa ratiba maalum ya Simba ili wacheze mechi hizo ili kuendana na kalenda ya TFF ilivyopanga kuwa ndani ya mwezi Mei wanataka ligi iwe imemalizika.
Amefunguka kuwa kuna fainali ya Kombe la Shirikisho 'FA' ambalo pia mshindi bado hajapatikana nalo fainali yake inapaswa kucheza.
Moja ya watu waliolalamikia Simba kuwa na viporo vingi mpaka sasa ikiwa na 11, ni Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye alieleza kama kuna upendeleo fulani unafanyika.
from SALEH JEMBE http://bit.ly/2IeCdL9
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
