Mbwana Samatta na Alikiba waja 'kampeni' kabambe tena
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mbwana Samatta anayecheza soka la kulipwa katika club ya KRC Genk nchini Ubelgiji, ameungana na msanii wa muziki wa kizazi kipya napia mchezaji wa Coastal Union ya Tanga, Alikiba na kuanzisha taasisi kwa ajili ya kusaidia jamii.
Taasisi hiyo ambayo imepewa jina la SamaKiba Foundation imedhibitishwa na Samata mwenyewe baada ya kuposti picha kwenye mtandao wa Twitter inayoonekana ni nembo rasmi ya taasisi hiyo yenye kauli mbiu ‘Rudisha tumaini kwa jamii”
Huu utakuwa ni mwendelezo wa kile walichokifanya Samatta na Alikiba mwaka jana mwezi June baaada ya kuandaa mchezo wa hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha zilizotumika kusaidia sekta ya elimu.
Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON

