Mkurugenzi wa Vodacom aachiwa huru


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Vodacom, Hisham Hendi na wenzake 8, wamefanikiwa kulipa faini ya Tsh. Bilioni 6.01 baada ya kukiri mashtaka yao.

Walishtakiwa kwa kuingiza, kutumia na kusimika vifaa vya mawasiliano, kugawa namba za simu, kupiga simu za kimataifa nje ya nchini bila leseni kutoka TCRA.

Mashtaka mengine ni kumiliki vifaa, kulaghai pamoja na mashtaka mawili ya kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 8.

Pamoja na Washtakiwa kupewa hukumu huyo ya kulipa faini ya Tsh. Bilioni 6.01, Mahakama hiyo imetaifisha mitambo na vifaa vyote vya mawasiliano vilivyotumika katika uhalifu huo.

Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON