Ripoti ya CAG yabaini madudu Hanang’
Na John Walter Manyara
Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonyesha mapungufu mbalimbali ambapo katika Halmashauri ya wilaya ya Hanang’ mkoa wa Manyara imepoteza Mapato ya ndani Zaidi ya Shilingi Bilioni 3.4
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Mapitio ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato ya ndani yalibaini mapungufu katika Halmashauri hiyo kushindwa kuwasilisha vitabu 425 vya kukusanyia mapato.
Imeendelea kueleza kuwa kuna Upotevu wa mapato ya ndani ya Halmashauri ya jumla ya shilingi bilioni 1.04 yaliyokuwa yanakusanywa na mawakala na Kutopatikana kwa nyaraka muhimu za makampuni ya mawakala wa ukusanyaji wa mapato kwa mikataba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.36
Ripoti hiyo ya (CAG) Mussa Assad iliyowasilishwa april 10.2019 mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake Jijini Dodoma imesema kuwa yapo Malipo Hewa ya Shilingi Milioni 73.45 katika Kandarasi za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji katika Halmashauri hiyo.
Aidha Ukaguzi maalumu umebaini kuwa fedha kiasi cha shilingi milioni 73.45 za Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Maji zililipwa kwa wakandarasi kama dharura bila kuwepo kazi za dharura huku Ukaguzi huo ukibaini kwamba hakuna ushahidi wowote wa kufanyika kwa kazi hiyo, na hivyo kudhihirika kuwa matumizi hayo ni hewa.
Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
