Askari wanaodaiwa kumuua mwanachama wa ACT wakamatwa

 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu saba kwa tuhuma za mauaji ya Said Salum Suleiman (32) mkazi wa Mwembemakumbi mjini Unguja.

Wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Suleiman ambaye alikuwa Katibu wa ACT-Wazalendo Tawi la Mwembemakumbu ni Askari wanne wa Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Maofisa watatu wa idara ya misitu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amesema Suleiman alipigwa risasi na Maofisa hao eneo la Mwembemakumbi.



Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON