Rais Magufuli ahuzunishwa na kifo cha Rais wa zamani wa Ghana
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ameonesha kuhuzunishwa na kifo cha aliyekuwa Rais wa Ghana Jerry John Rawling.
kupitia ukurasawa wake wa twitter Rais Magufuli ameandika “Nimehuzunishwa na taarifa za kifo cha Rais wa zamani wa Ghana Jerry John Rawlings, salamu zangu za rambirambi kwa Rais wa Ghana Nana Akufo- Addo na Watu wote wa Ghana kwa kumpoteza Jerry Mwamba wa Afrika, apumzike kwa Amani, Amen”.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Ghana Rais huyo amefariki kutokana na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.
Jerry Rawlings alizaliwa Juni 22, June, 1947 ameaga dunia katika Hospitali ya Korle Bu Teaching, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON
