Biden asema kipindi cha mpito kinaendelea licha ya Trump kukataa matokeo


Rais mteule wa Marekani Joe Biden amesema mchakato wa kipindi cha mpito unaendelea vyema licha vizingiti kutoka kwa utawala wa Rais Donald Trump, ambaye amekataa kukubali ushindi wa Biden na kuupinga mahakamani. 

Akizungumza katika kikao cha wanahabari jana, Biden alisema tayari wameanza utaritibu wa makabidhiano ya madaraka na kuwa hatua ya Trump kukataa kukubali kushindwa haibadilishi chochote. 

Waziri wa Mambo ya Kigeni Mike Pompeo alisema kutakuwa na utaratibu mzuri wa kukabidhi majukumu kwa muhula wa pili wa utawala wa Trump, alipoulizwa ni lini Wizara ya Mambo ya Kigeni itaanza kuukabidhi majukumu utawala wa Biden.

 Lakini baadaye akasema makabidhiano yataamuliwa na kile ambacho watu waliamua wakati kura zote zitakapohesabiwa. Biden alitangazwa mshindi na karibu televisheni zote za Marekani. 

Viongozi wengi wa ulimwengu wakiwemo wa Ujerumani, Uingereza na Ufaransa wamemtambua Biden kuwa rais mteule na kumpongeza kwa njia ya simu.



Chanzo MUUNGWANA BLOG
ILI KUWA WA KWANZA KUPATA HABARI USISAHAU KU LIKE PAGE YETU,BONYEZA LIKE BUTTON